#VisibleWikiWomen 2024

Rangi katika mapambo ya kichwa cha Visible WikiWomen zimeundwa kutokana kwa maumbo ya mimea ya kikaboni.

2024 ni mwaka wa 7 na toleo la kampeni ya #VisibleWikiWomen.

Kwa miaka sita iliyopita, tumeleta pamoja kundi la washirika na marafiki duniani kote ili kutengeneza picha za wanawake jumuiya, hasa watu weusi, kahawia, wa kiasili, na watu wa jinsia transijenda na jinsia ya walioghairi uwili, kuauniwa na Wikipedia na kupatikana katika mtandao. Tunajivunia na kushukuru kwa maelfu ya picha ambazo kampeni imeleta mtandaoni na matukio yote, tafakari na uingiliaji kati ambao tumefanya kupitia #VisibleWikiWomxn.

Bofya hapa ili kujiunga!

Maarifa na michango ya wanawake kwa ulimwengu zimedhalilishwa kwa njia nyingi. Tunapochunguza ukosefu wa wanawake mtandaoni, Wikipedia ni wakala mzuri wa kueleza kwa nini hili ni suala nyeti. Chini ya ¼ ya wasifu wa Wikipedia huwakilisha wanawake. Wasifu mwingi wa wanawake muhimu na wenye ushawishi haupo au haujakamilika.

Mara nyingi, wasifu wa wanawake hauna picha. Tunakadiria kuwa chini ya 20% ya nakala za Wikipedia za wanawake muhimu zina picha. 21% pekee ya picha zinazoonyesha wanadamu kwenye Wikimedia Commons zinawakilisha wanawake (kulingana na https://humaniki.wmcloud.org).

Nyuso za wanawake zinapokosekana kwenye Wikipedia inachangia kudhalilishwa zaidi . Watu nusu bilioni husoma Wikipedia kila mwezi, na iko katika tovuti 10 zinazotembelewa zaidi duniani. Kwa maneno mengine, mapungufu kwenye Wikipedia yana athari kubwa kwenye mtandao mpana na ulimwenguni.

Mchoro wa safuwima unaonyesha asilimia ya wasifu wa wanawake kwenye Wikipedia (25%), wakati mchoro mwingine unaonyesha asilimia ya nakala za wanawake walio na picha (20%).

Mapengo hayo ya mwonekano kwenye Wikipedia na mtandao huongezeka hata zaidi wakati wanawake ni weusi, kahawia, wa jinsia tofauti, walemavu, wa kiasili, si wembamba, au wapo kwenye makutano ya dhuluma hizo nyingi na udhaifu.

Mwaka 2023 ulikuwa wa kufana sana kwa kampeni yetu. Tulikusudia kusherehekea mtandaoni wingi wa maumbile ya miili yetu chini ya mandhari ya #BodyPlurality #CuerposPlurales #CorposPlurais #Imizimba: Kusherehekea maumbile yetu ya kipekee viwiliwili vyetu na tunavyojitambulisha. Kwa pamoja tulikidhiri lengo letu na kuleta zaidi ya taswira elfu tatu (3000+) kwa Wikimedia Commons za miili na viwiliwili tofauti, rangi na maumbile mbalimbali; Miili inayomiliki ajira tofauti, inayomiliki spoti, inayomiliki jukwaa tofauti na inayomiliki mitaa yetu na kuleta utukufu wa wingi wa maumbile ya miili tunaokusudia kuona mtandaoni na katika Wiki.

Tungali tunatafakari maana ya #BodyPlurality (Wingi wa maumbile) kwetu sisi na kwa marafiki, na kwa washiriki wetu na kwa wanaotuunga mkono na kwa wote tunoawatumikia kwa kazi hii ya upinzani kwa “vigezo vya urembo” na vima vya miili ipi inayo stahiki kukubalika, kusherehekewa na kuonyeshwa. Roho ya Ufeministi wetu na siasa zetu za uhuru wa maumbile na yote tuliyojifunza yatuhamasisha na ndio moyo wa #VisibleWikiWomen.

2024 pia ina msiba wa ghadhabu ya pamoja na huzuni huku zana za mifumo zikiendelea kuwa silaha dhidi ya miili yetu, jamii zetu, na ardhi zetu.

Kampeni ya #VisibleWikiWomen mwaka huu inasisitiza kwamba mapambano yetu yote yana umoja, na kuna Uwingi katika Upinzani wetu, kama mfenisti wa ajabu wa haki za binadamu na mtetezi wa ardhi  Berta Cáceres alivyosema. Tukiongozwa na mafundisho ya Audre Lorde kwamba hatuishi maisha ya suala moja, kutoka Sudan hadi Palestina, kutoka kwa haki ya uzazi hadi haki ya ujuzi, haki ya hali ya hewa, kampeni ya 2024 itaangazia picha na hadithi za kazi ya ukombozi wetu wa pamoja:

  • Waongozi-fikra na wajenzi wa amani  kama Margo Okazawa-Rey na Gwyn Kirk, ambao walikuwa muhimu katika kutunga “Dira ya Kifeministi ya Usalama wa Kweli“.
  • Madres y Abuelas de Plaza de Mayo, mwanaharakati maarufu wa haki za binadamu wa Argentina ambao maandamano yao ya amani ni ishara ya kimataifa ya haki na kumbukumbu maarufu.
  • Mawimbi yanayoendelea ya waandamanaji wanaopinga unyanyasaji wa kijinsia kutoka Argentina, wakihamasishwa kutoka Argentina chini ya alama ya reli #NiUnaMenos, Kenya wakiwa na #StopKillingWomen, na  #StopFGMInGambia huko Gambia.
  • Watafutaji haki kwa wanawake weusi kama Marielle Franco, wanawake wa kiasili na watetezi wa ardhi kama Berta Cáceres, na wanaharakati wa jinsia tofauti kama vile Alejandra Ironici, na wengine wengi ambao maisha yao yanaendelea kukuza mapambano yetu mengi.
  • Jamii ya Upinde na wanaharakati nchini Uganda, Ghana, na kila mahali ambapo sheria za chuki ya ujinsia kuchu (homofobia) na upunguzaji wa haki za binadamu wa mrengo mkali wa kulia unazidi kuota mizizi.
  • Watu kuchu na wa jinsia transijenda Dalit ambao ni wasomi, wanahabari na wanaharakati wanaoendelea kupindua tabaka, jozi na kanuni za kawaida ili kutoa nafasi ya matumaini, furaha na upendo.
  • Wafemenisti na wanawake katika  Palestina, Sudan, Kongo, Sahara Magharibi, na kwingineko, ambao wanafanya uharakati katika hali mauaji ya kimbari na vita, wakituonyesha upinzani wa wanafeministi, ukombozi, matumaini, na mshikamano katika vitendo.
Kolagi ya watetezi wakuu wa wanawake walioongoza mada ya mwaka huu.
Kolagi ya VisibleWikiWomen 2024. Picha YoulendreeAppasamy, kutoka Berta Cáceres picha, Margo Okazawa-Rey na Gwyn Kirk picha, Alejandra Ironici picha, Marielle Franco picha, Waandamanaji wanaounga mkono Palestina picha na picha ya muandamanaji wa Sudan, CC BY-SA 4.0, kupitia Wikimedia Commons.

Tuko katika hali ambayo vurugu, migogoro na vita vimekuza sura mbaya zaidi ya ufundishaji wa ukatili, unaochochewa na teknolojia, vyombo vya habari, na ulimwengu wa kidijitali unamilikiwa na ajenda za ubepari na ubaguzi wa rangi. Popote wanawake jumuiya walipo, wanaathiriwa zaidi na makali ya migogoro na vurugu. Lakini wanawake jumuiya pia wanafanya uharakati bila kuchoka katika mshikamano na upinzani dhidi ya mifumo ya ukandamizaji — ukoloni, mfumo dume, ukuu wa wazungu, ubaguzi wa rangi, ukabila, chuki ya ujinsia kuchu (homofobia), chuki ya watu transijenda (transfobia), ubepari, tata ya viwanda vya vita, na mengine. Ni lazima tutambue tulipo katika historia na tuchangie juhudi za ufeministi kote duniani ili kuweka kumbukumbu ya ghadhabu yetu, kusherehekea ubinadamu wetu kamili, na kuangazia hadithi na picha za upinzani wa kefeministi, ukombozi, muungano na amani.

Na mada yetu ya 2024: “Uwingi katika Upinzani wetu: Mshikamano wa kifeministi, ukombozi, na amani”

Tunawaalika washirika wetu, marafiki, na wenzetu katika mapinduzi ya uhuru wetu wa pamoja kwenye kampeni ya 2024 #VisibleWikiWomxn:

  • Kufanya dua na kuunda kumbukumbu zetu za ufeministi na kushuhudia mawezekano ya itikadi kali za mshikamano na haki,
  • Kutambua athari za kijinsia za vita na migogoro, kufanya kazi ya wajenzi wa amani na watetezi wa haki za binadamu ionekane kupitia picha zinazowakilisha nguvu, ushupavu, heshima, utu, maandamano na mshikamano,
  • Ili kusherehekea njia nyingi za wanafeministi huunganisha mapambano mengi ya ukombozi katika kukabiliana na aina zinazoingiliana za ukandamizaji wa kimfumo. Kwa sababu hakuna mtu aliye huru hadi kila mtu awe huru.

Lengo letu la toleo hili la saba la #VisibleWikiWomen ni kuleta picha zingine 7000 za wanawake na watu binafsi wa jinsia ya walioghairi uwili kwa Wikimedia Commons, maktaba kubwa ya media titika kwa miradi yote ya Wikimedia, ikijumuisha matoleo ya lugha +300 ya Wikipedia.

Kwa mara nyingine tena, tutaangazia kuongeza idadi ya picha za watu Weusi, Wakahawia, Wakiasili, Wanawake wa jinsia transijenda na watu wa jinsia ya walioghairi uwili wenye ushawishi mkubwa ambazo zinapakiwa kwenye Wikipedia kama sehemu ya kampeni ya  #VisibleWikiWomxn.

Ili kufikia lengo hili, tunaalika – mashirika ya wanawake na wafeministi, taasisi za kitamaduni na kumbukumbu, wahariri wa Wikipedia, vikundi vya watumiaji, tawi, na mtu yeyote ambaye angependa kuchangia kwa wingi wa wanawake na watu wa jinsia ya walioghairi uwili mwonekano na uthibitisho wanaostahili. Tunafurahi kushirikiana tena na marafiki, washirika na washiriki njama wa mwaka uliopita, na kuwakaribisha washirika wapya kutoka duniani kote.

#VisibleWikiWomen sasa ni kampeni ya kila mwaka, lakini sherehe na ukumbusho fulani wa mwaka zinaweza kuwa kama nyakati maalum za kushiriki. Tunataka kuangazia matukio muhimu yafuatayo kwa jumuiya zetu kwa mwaka mzima:

  • Machi: Siku ya Kimataifa ya Wanawake #8M
  • Aprili: Mwezi wa Historia ya Dalit, Siku ya Uhuru nchini Afrika Kusini
  • 1 Mei: Siku ya Wafanyakazi, wakati wa kusherehekea wanawake wote katika maeneo yao ya kazi
  • Juni: Mwezi wa Fahari wa Jamii ya Upinde
  • Julai: #MweziwaFahariyaWalemavu
  • Tarehe 31 Agosti: Siku ya Kimataifa ya Watu Wenye Asili ya Kiafrika na Mwezi wa Wanawake [SA]
  • 5 Septemba: Siku ya Kimataifa ya Wanawake wa Asili
  • Septemba 28: Siku ya Kimataifa ya Utoaji Mimba kwa Usalama
  • Oktoba: Mwezi wa Historia ya Watu Weusi [Uingereza, Ireland, Uholanzi]
  • Tarehe 25 Novemba hadi 10 Desemba: Siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia
  • Na zaidi…

Unaweza kujiunga na kampeni ya  #VisibleWikiWomen mwaka mzima, kwa kukusanya na kupakia picha za ubora katika kikoa cha umma, au chini ya leseni ya bure, kwa Wikimedia Commons chini ya kitengo cha VisibleWikiWomen. Picha hizi zinaweza kuwa picha au michoro ya wanawake, pamoja na picha za kazi zao, na idhini sahihi.

Kando na kupakia picha kwa Commons, unaweza pia kushiriki katika kampeni kwa:

  • Kukaribisha watu au kuhudhuria mikusanyiko katika jumuia yako ambapo picha zinaweza kupigwa au kupakiwa
  • Kuwachilia picha zako zilizopo za wanawake na watu wa jinsia ya walioghairi uwili ya leseni za bila malipo
  • Kuunda vielelezo na michoro
  • Kukuza na kutangaza mradi huu kwa kueneza habari kuuhusu na kutumia alama za reli #VisibleWikiWomen, #VisibleWikiWomxn,#LuchasMultiples #OurPluralResistance#WomenofColors, #on Facebook, X, na Instagram.
  • Kuratibu na kukaribisha tukio la mtandaoni na Whose Knowledge? kuleta kampeni kwa jumuiya zako.
  • Kuunda kona ya kutetea haki za wanawake katika matukio yako ya umma, kwa kusakinisha kibanda cha picha cha #VisibleWikiWomen.

Na pengine mengi zaidi! Tungependa kukuona ukitoa mawazo mapya ambayo yana maana kwako na jumuiya zako.

Iwapo unahitaji usaidizi wa ziada kwa ajili ya kushiriki katika kampeni, tafadhali tutumie barua pepe kwa visiblewikiwomen@whoseknowledge.org.

‣ Saidia kufanya kampeni yetu iwe ya lugha nyingi kwa kutafsiri ukurasa wetu wa Meta, seti ya rasilimali, na kurasa za kampeni za tovuti yetu katika lugha tofauti. ‣ Tengeneza orodha za wasifu wa wanawake wa Wikipedia bila picha (kulingana na nchi, kwa kazi, kwa karne, kwa shughuli) ili kuongeza ufahamu wa pengo la kuona jinsia na kuunda changamoto za kuvutia kwa washiriki. ‣ Andika nakala mpya ya Wikipedia iliyochochewa na picha ya wanawake  “yatima” (picha isiyo na nakala) na utumie picha hiyo kuielezea.

Eneza neno

‣ Tengeneza na ushiriki: chagua picha unazopenda, na ukichanganye kwa hiari na maandishi na sanaa ya kutia moyo, na uishiriki na lebo za #VisibleWikiWomen na/au #LuchasMultiples #OurPluralResistance.

Kuunga mkono kampeni

‣ Ikiwa wewe ni shirika la wanawake, taasisi ya kitamaduni na kumbukumbu, vyombo vya habari au shirika lingine linalowezekana la washirika, kuwa mshirika wa kitaasisi ‣ Ikiwa wewe ni mtu ambaye umeunganishwa na washirika watarajiwa (kama waliotajwa hapo juu), tafadhali watambulishe kwenye kampeni! Ikiwa umeunganishwa na wafadhili ambao wanaweza kufadhili na kuunga mkono kampeni hii, tafadhali walete kwenye kampeni! ‣ Iwapo ungependa kujitolea kuunga mkono kampeni ya mwaka huu, tuandikie mstari katika visiblewikiwomen@whoseknowledge.org. Daima kuna nafasi ya kukaribisha washirika wapya kila mara! ‣ Ikiwa ungependa kusaidia kifedha kampeni ya mwaka huu, bofya hapa:

Mnamo 2018, tulizindua toleo la majaribio, la VisibleWikiWomen likifuatiwa na kampeni zingine tano zilizofaulu mnamo 2019, 2020, 2021, 2022, na 2023. Vivutio kutoka kwa kampeni yetu ya mwaka jana ni pamoja na:

  • Mnamo 2023, tulianza mwaka wa 6 wa kampeni yetu ya #VisibleWikiWomen    wambayo tulizindua tarehe 27 Aprili 2023 chini ya mada #BodyPlurality #CuerposPlurales #CorposPlurais: Kuadhimisha upekee kamili wa ukubwa wa miili yetu ya wingi, maumbo na utambulisho mtandaoni. Tulikusanya takriban marafiki 30 na washirika wetu kwa ajili ya uzinduzi. Kufikia Desemba 2023, zaidi ya picha 3000 zilishirikiwa kupitia kampeni, na kupita lengo letu la faili 2500. Zaidi ya nambari, baadhi ya matumizi ya picha ni maalum sana kwetu, kama vile katika makala ya Wikipedia ya Uhispania Día Internacional de las Mujeres Rurales, na  Wiki Loves Fashion NL flyer.
  • Kwa mara ya kwanza, mnamo 2023, tuliandaa shindano la sanaa na picha chini ya mada, “Kuchambua wingi wa miili katika spoti” kama njia ya kusherekea miili ya wanawake jumuiya na watu jinsia ya walioghairi uwili katika michezo kwa kuweka sauti zao, taswira, hadithi, na uzoefu katika michezo katika utofauti wao wote, wingi, na utukufu.
  • Pia tulishirikiana na jumuiya yetu katika mashindano mengi zaidi mwaka mzima. ¡Alto! Mujeres Trabajando, kwa ushirikiano na sura za Wikimedia katika LAC, waliwahimiza washiriki kupinga dhana potofu za kijinsia mahali pa kazi. Ilustratona Mulheres Visíveis, iliyoandikwa na Wiki Editoras Lx, iliwaalika wasanii kuunda vielelezo vya wasifu waliochaguliwa, hasa wanawake weusi wa ulimwengu wa lusophone.
  • Jumba la picha la #VisibleWikiWomen lilikuwa sehemu ya matukio mbalimbali duniani, huko Costa Rica, Botswana, Singapore na Brasília. Kulingana na matumizi haya yote, tumeunda kwa uangalifu muundo wa fomu ya idhini, inayopatikana kama nyenzo kwenye Wikimedia Commons kwa English na Spanish.
  • Data mwafaka ni mada ya kisiasa na kiutendaji ya wanawake, kwa hivyo tuliendelea na mazungumzo kuihusu katika kipindi cha Wikimania. Tulifanya warsha ya data mwafaka ya #VisibleWikiWomen wakati wa Mkutano wa Wanawake wa Wiki huko Wikimania tarehe 16 Agosti.
  • Kama sehemu ya kampeni ya UN #16days kila mwaka dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia, tulishirikiana na Wikimedia Chile na Wikimedistas de Uruguay katika  changamoto ya uhariri. Lengo lilikuwa kupanua na kuboresha maudhui kwenye Wikipedia kwa Kihispania ili kufanya kazi muhimu ambayo wanawake watetezi wa haki za binadamu hufanya ionekane, mara nyingi kwa rasilimali chache na chini ya vitisho vikali.

Ikiwa hujawahi kupakia picha kwenye Wikipedia au Wikimedia Commons hapo awali, usijali, tumekushughulikia! Tumeunda seti hii ya nyenzo ya #VisibleWikiWomen, ambapo utapata maagizo na ushauri wa vitendo kuhusu jinsi ya kutumia Wikiverse, hasa jinsi ya kutumia Wikimedia Commons.

Nyenzo ya Jinsi ya kupakia picha ili kuwafanya wanawake waonekane kwenye Wikipedia na Mtandao ni muhimu sana kwani itakuongoza katika mchakato wa kupakia picha za kampeni hii.

Rasilimali zingine zinazohusiana na za kusaidia ni:

…na kama unahitaji msukumo, hapa kuna  orodha ya makala ambazo hazina picha za wanawake kwenye Wikipedia.