Kuaga kampeni ya #VisibleWikiWomen: hadithi na tafakari

22 August 2021

#VisibleWikiWomen 2021 imefikia tamati. Katika miezi mitatu ya kampeni, pamoja na washirika wetu na jamii zetu, tumezipitia changamoto mpya, ubunifu, vipaji vya muungano wa kifeministi picha za fahari za wanawake kutoka kote ulimwenguni.

Janga la Covid-19 ulimwenguni lilituathiri sisi, washirika wetu na jamii, na #VisibleWikiWomen kwa njia nyingi. Hasa, iliathiri upakiaji wa picha kutoka kwa taasisi za GLAM na washirika wetu wengine wa Wikimedia. Pia ilizuia ushiriki wa jamii nyingi, haswa zile kutoka nchi za kusini mwa dunia (kimaendeleo) ambao wameathiriwa vibaya na janga hilo.

Uhalisia wa changamoto hii, wa kutisha na mara nyingi wa kuchosha ulihitaji ubunifu mwingi na uthabiti kutoka kwetu na jamii zetu. Tulitegemea hekima ya marafiki wetu wa kike na washirika kutoka  Association for Women’s Right and Development (AWID) kuchagua mada ya kampeni ambayo ilituhamasisha na kututia moyo.

“Uhalisia wa Kifeministi: Kuishi Ukweli wa Kiupinzani na Kiukombozi”

Tulizingatia kusherehekea wanawake /jamii transijenda/jamii ya walio ghairi jinsia uwili – ambao huunda uhalisia wetu wa kifeministi kwa kuishi kimapinduzi, kungatua mifumo ya ukandamizaji na kutafuta ukombozi na haki kwa wote.

#VisibleWikiWomen 2021 ilileta picha zaidi ya 1700 kwa Wikimedia Commons, ikionyesha kurasa katika lugha 38 tofauti za Wikipedia. Nambari hizi, hata hivyo, hazisemi hadithi kamili; kwa kweli, hakuna mtu bora kuliko marafiki wetu na washirika ambao walijiunga na kampeni kushiriki kile #VisibleWikiWomen ilimaanisha kwao na jamii zao. Tunakualika kuhamasishwa na ujifunze kutoka kwa wanawake ambao waliunda uhalisi wao wa kifeministi ilhali kuwepo katikati ya janga la ulimwengu.

#VisibleWikiWomen 2021 kupitia sauti za watetezi watano wa utambuzi wa wanawake

Jiunge na Catalina Gutierrez, Justina Aina, Modak Basudha, Ruby Damenshie-Brown, na Selva Mustafa, ambao watakusimulia hadithi ya #VisibleWikiWomen 2021.

Mtaalamu was maswala ya jinsia na uendelevu kutoka Jamhuri ya Dominika. Catalina Gutierrez amefanya kazi na mashirika ya serikali, ya kimataifa, ya kielimu, vyombo vya habari na sekta ya kibinafsi, pamoja na Umoja wa Mataifa, kukuza usawa wa kijinsia.

Womxyn mfanisi mwenye asilia za Uingereza-Nigeria. Kama muigizaji, mbunifui, mtaalam wa sauti, mshairi na mtayarishaji, Justina Aina anapata motisha kwa kutafakari hadithi mpya na miundo mpya ya uzalishaji ambazo zinapaswa kupewa maua zaidi, mtandaoni na nje ya mtandao.

Mhandisi kwa taaluma na mkufunzi mwenye shauku kutoka Afrika Kusini. Modak Basudha anafanya kazi ya kujenga jamii ya wanawake ambao hadithi zao zinasikika na kutambuliwa. Yeye ni mtetezi wa jamii endelevu ambapo sauti zote husikika na kutambuliwa.

Mtetezi wa jinsia na aliye na shauku kuhusu uwazi wa elimu na nyenzo. Ruby Damenshie-Brown anafanya kazi katika Open Foundation West Africa (OFWA), ambapo anakuza ufikiaji na uwazi wa elimu kupitia miradi tofauti huko Ghana, nchi yake ya asili.

Mwanachama wa The Elephants Trail (kikundi kinachofadhiliwa na Lankelly Chase) na mtaalam wa hematolojia kama taaluma. Kama mtu aliyebaguliwa kutoka Greater Manchester UK, Selva Mustafa ana ari ya kweli kufanya sauti zingine kusikika ili watu waweze kuishi maisha ya ya kuridhisha katika mazingira mazuri ya kufanya kazi.

Kuongeza Kutambulika Kwa Wanawake Mtandaoni Kwa Kupea Kiupa Umbele Jamii za Kusini Kimataifa

Tukijipa moyo na mada yetu ya “Uhalisia wa Kifeministi”, tulifanya bidii zaidi kuipa kiupa umbele jamii zetu za Kusini Kimataifa wakati wa toleo hili, haswa jamii zetu za bara la Afrika. Tuliajiri mratibu wetu wa kwanza anayeishi Afrika, Pamela Ofori-Boateng kusaidia washirika wetu wa Afrika na kuleta washiriki wapya kwenye kampeni. Kama matokeo, tumeongeza idadi ya picha zinazotambua wanawake wa Kiafrika wakati wa kampeni hii, ikilinganishwa na matoleo ya awali.

Pia tuliunga mkono uzoefu wa pamoja wa mafunzo kwa kuongoza na kuongoza warsha juu ya jinsi ya kupakia picha kwa Wikimedia Commons. Tulishirikiana warsha mbili mtandaoni na washirika wetu AWID na World Pulse, wote wakiwa mitandao ya kimataifa ya kifeministi na kuwezesha safu ya warsha katika “Greater Manchester Narratives Lab”, hadithi ya utamaduni na mchakato wa haki ya maarifa.

#VisibleWikiWomen warsha na jamii ya AWID

Washiriki wengi waliohudhuria hafla hizi walikuwa hawajawahi kupakia picha kwa Wikimedia Commons, na wengi walikuwa hawajasikia juu ya harakati ya Wikimedia na juhudi zake za nyenzo ya wazi. Kila hatua ya mchakato huo ilikuwa mpya kwao. Catalina Gutierrez anaelezea kuwa wenzao walijadili kwa kina ni maelezo gani yanayofaa kwa picha inaweza kuwa, kwa Kiingereza na Kihispania. “Mara tu tukipakia picha hiyo, tuliiangalia na ikaonekana kwenye injini ya utaftaji. Ilikuwa tukio la furaha kwetu sote, ”alisema.

Kwa mara ya kwanza mwaka huu, tumejaribu wazo la kusaidia waandaaji wa hafla moja kwa moja na rasilimali fedha na ujuzi, pamoja na rasilimali za nyenzo ambazo tulikuwa tumechapisha hapo zamani. Mwisho wa kampeni yetu, waandaaji wetu wenyeji walishiriki hafla sita za kiwango cha kitaifa #VisibleWikiWomen mtandaoni: nne Afrika (Ghana, Kenya, Rwanda na Tanzania), na mbili huko America ya Kusini (Argentina na Uruguay). Licha ya kuunda na kuongeza uwezo na ujuzi na utaalam, hafla hizi na warsha zilitumika kama fursa za kutafakari juu ya pengo la kijinsia katika Wikipedia na athari zake kwenye mtandao mpana.

Wakati wa semina hizi za mtandaoni, washiriki walishiriki kwa shauku wakati wa vikao vya kuzuka:

“Funzo  moja kuu ya kitaalam kutoka kwa warsha hiyo ilikuwa uwezo wa timu katika Whose Knowledge? kueleza shida au pengo na jinsi kampeni hii inataka kuziba ufa huu na kisha kujenga uwezo wa washiriki kwa kuwapa uzoefu wa kupakia picha zao kwenye Wikimedia Commons. Kujumuisha vyumba vya kando ili kuwezesha mchakato huu kulihakikisha kuwa washiriki wote wanapata msaada unaohitajika. Hii ni muhimu na kitu ambacho nadhani nitajumuisha katika siku zijazo wakati wa kuandaa semina kama hizo. “

— Ruby Brown

Kiwango cha nishati ambacho washiriki walijiunga na kila hatua kinaonyesha mtazamo wa umuhimu wa mipango ya utambuzi. “Ni dhamira ya maisha yangu kuhakikisha wanawake wengi wanasikilizwa na kwamba kuna wanawake zaidi katika majukumu ya kufanya maamuzi katika kila kamati ulimwenguni,” alisema Modak Basudha, kutoka World Pulse

Katika athari nyingine inayoenea ya ukosefu wa usawa, nafasi za mtandaoni kama Wikipedia zinaendeleza mapengo ya kijinsia katika nyenzo zao. Asilimia 20% tu ya wasifu kwenye tovuti hii – ambayo inabaki kuwa moja ya kutumika zaidi kwenye wavuti – inawakilisha wanawake, na wasifu hata wachache wana picha za wasifu zinazoonyesha yao. Pengo la kijinsia kwenye Wikipedia ni la kina na huenda zaidi ya uwakilishi na kutoonekana kwa wanawake katika nyenzo. Wachangiaji wa Wikipedia pia ni wanaume wazungu hasa kutoka nchi za Ulaya na Amerika Kaskazini na wastani wa asilimia 10 tu ya wahariri hujitambulisha kama wanawake.

#VisibleWikiWomen inachukua msimamo dhidi ya aina hizi za udhalimu wa maarifa, ambayo husababisha kazi ya wanawake kupuuzwa na maarifa za jamii zilizotengwa nyenzo zao na maarifa yao kupuuzwa. Ruby Brown alisifu mradi huu kama suluhisho kwa pengo la jinsia. “Inawapa wanawake wengi nguvu ulimwenguni kushinikiza ajenda hii na kuboresha maelezo” alisema, baada ya kuhudhuria warsha iliyoandaliwa na World Pulse na Whose Knowledge? “Kampeni hii inahimiza wanawake kuwa sehemu ya Historia, kuwa wahusika wakuu na kuongoza uwakilishi sahihi wa vitendo vyao kupitia maandishi na picha zilizoshirikiwa,” alisema Catalina Gutierrez, ambaye alihudhuria hafla hiyo hiyo.

Justina Aina, baada ya warsha na Maabara ya Greater Manchester Narratives, alisema:

“Kuwa na hadithi [za wanawake] zilizonaswa na viungo vya kuimarisha maarifa ni muhimu sana kwani, wakati mwingi, wanawake waliotajwa “hawawapigi honi zao” wenyewe. Pia ni njia ya kuhakikisha kuwa maboresho ya jamii na uchochezi vinaweza kufuatiliwa kwa vyanzo vyao na watu wanaweza kushikilia hadithi zao. “

#VisibleWikiWomen warsha na jamii World Pulse

Kushinda changamoto na kujifunza pamoja

Katika kampeni yetu ya mwaka wa pili katikati ya Covid-19, jamii zetu, washirika na wasaidizi bado walihisi makali ya janga hilo, kama ilivyoelezwa na Modak Basudha. “Kanuni hapa zimepunguza mawasiliano yangu ya ana kwa ana mara nyingi kama nilivyopenda, lakini hata hivyo polepole kazi bado inaendelea. Na nitashukuru milele kwa warsha zilizonipa mwongozo kwa maono niliyokuwa nayo” Mkurupuko mpya na anuwai za virusi ziliibuka, na kuongeza pengo la usawa kati ya kusini na kaskazini duniani haswa kwa masuala ya upatikanaji wa misaada, chanjo, huduma ya afya, msaada wa kiuchumi na kijamii. Katika hali hii, imekuwa ngumu kwa washiriki wengi wa mitandao yetu kuwekeza juhudi na wakati katika kuandaa kampeni kwao.

Licha ya hayo, washiriki wengi walichukua hatua zao za kwanza kuhariri Wikimedia Commons kwenye warsha za #VisibleWikiWomen, ilhali wengine walishangazwa na uwezekano wa uzalishaji na ushirikiano:

“Ninachokuchukua kutoka kwa vikao hivi ni kwamba Wikipedia ina ushirika na uelewaji kuliko nilivyoongozwa kuamini”

– Justina Aina

“Jambo moja la kiteknolojia nililojifunza ni jinsi ya kuhariri katika Wikimedia Commons. Sikuwa nimewahi kusikia hata kuhusu Wikimedia Commons na sasa najua jinsi inavyofanya kazi. Nina maoni tofauti kabisa ya Wikipedia ambapo nilidhani chochote kinaweza kuhaririwa kwa urahisi na bila hundi, sasa najua !! ”

– Selva Mustafa

Kama matokeo ya kampeni hii, zaidi ya wahariri wapya 40 walijiunga na jamii ya Wiki na tunatarajia zaidi wataendelea kujiunga. Washiriki wana uwezekano wa kufunza jamii zao yale waliyojifunza, kama Selva Mustafa alituambia.Pia nitashiriki yale niliyojifunza na wenzangu wengine kwa sababu ujuzi wa aina hii unahitaji kuenezwa na wao ni jamii bora wa jambo hili!”.

Matumaini na ndoto zetu kwa #VisibleWikiWomen 2022

Katika mwaka ujao, tuna hamu ya kuunga mkono zaidi uongozi wa washirika wetu na jamii kuandaa hafla zao za #VisibleWikiWomen, haswa kwa kuunda rasilimali nyingi za lugha na media za kutumika kwa kampeni.

Tunatarajia kushirikiana na mitandao zaidi ya kifeministi na taasisi za GLAM kutoka kusini mwa dunia na kuunda nafasi salama na zenye furaha kwa jamii zetu kujifunza kuhusu dunia ya wiki na kutafakari juu ya haki ya maarifa na pengo la kijinsia katika Wikipedia.

Kama Justina Aina alisema, alipoulizwa juu ya jinsi alivyohisi kushiriki katika kampeni hii:

“Inanifanya niwe na tumaini kuona idadi kubwa ya wanawake kwenye Wikipedia na kwenye mtandao.”

Sisi pia, tuna matumaini ya siku zijazo ambapo wanawake wanatambulika kweli na kwa usawa na kusherehekewa mtandaoni. Tunashukuru sana washiriki wengi, washirika na jamii, ambao wamejiunga nasi mwaka huu kutoa hatua nyingine kuelekea siku zijazo za pamoja.

Related Posts

Sorry, no posts matched your criteria.

Author Profile